contributor

Diamond Platnumz - Utanipenda



0 comments:

Mr blue ft Dunga _Baki Na Mimi (New audio song)



0 comments:

Why Do We Fall - Motivational Video



0 comments:

Hii ya magereza 9 duniani kubadilishwa kuwa hoteli kubwa imenifikia, Africa ipo moja tu!




Nimekutana na stori moja kwenye mitandao inayohusiana na magereza ya zamani ya wafungwa, yamekusanywa magereza 9 ya sehemu mbali mbali duniani na kubadilishwa kuwa kitu tofauti kabisa, na ukiyaona hutoamini kuwa majengo hayo yalishawahi kuwamagereza ya wafungwa!
Kwenye yale maeneo ambayo Serikali waliacha kuyatumia kama maeneo ya magereza ya wafungwa yamechukuliwa na kubadilishwa kuwa hoteli au shule mtu wangu, majengo ni yale yale sema ubunifu mdogo tu umetumika kuyageuza majengo hayo kuwa sehemu ya vivutio kwa watalii.


Na kwa msaada wa teknolojia ya kisasa kabisa sehemu hizi zimegeuzwa kuwa sehemu nzuri sana, zenye mvuto na kama ukitembelea maeneo hayo bila kujua historia ya sehemu hiyo itakuwa vigumu sana kwa wewe kujua kuwa jengo au eneo hilo lilikuwa lawafungwa magereza.
Hapa chini nimekusogezea picha 9 za maeneo na magereza mbali mbali duniani ambayo kwa sasa zinaweka headlines tofauti na miongoni mwa picha hizi kuna moja kutokaLagos Nigeria iliyoweka headlines


Centro Cultural Antigua Carcel – Le Crac Hotel; hili jengo lilikuwa la wafungwa magereza  Spain.
Hii ni Louviers Music School iliyopo Ufaransa lakini kabla ya mwaka 2011 jengo hili lilikuwa la wafungwa magereza.

 Cultural Park of Valparasio ni hoteli iliyopo China na kabla ya mwaka 1999 jengo hili lilitumika kama gereza la viongozi kwa kisiasa.

 Hii hoteli inaitwa Four Seasons Istanbul at Sultanahmet ipo Turkey mtu wangu lakini napo palishawahi kuwa sehemu ya kuhifadhia wafungwa

 Pentridge Prison ipo Australia lakini wenyewe hajabadilisha vitu vingi sana toka mwaka 1999 ila ni miongoni mwa hoteli zinazolaza watu wengi sana.


Museum of Belize ipo kaskazini mwa Marekani kwenye mji mdogo uitwao Belize City, na kabla ya mwaka 2002 jengo hili lilitumika kuhifadhi wafungwa.
Freedom Park Nigeria na jengo hili kabla ya mwaka 2010 lilitumika kama gereza la wafungwa.

Laurel Hill, Virginia nayo kabla ya mwaka 2001 palitumika kama gereza la watu wa Usalama.


Hostel Celica, wenyewe wanakupa ile mandhari halisi ya gerezani na palishawahi kuwa gereza la wanajeshi.

source>millardayo.com

0 comments:

Man Selecting Cobras For Snake Show




0 comments:

Kampuni ya kwanza kuunda magari kutoka Africa




0 comments:

Find us on facebook