contributor

SIKU YA HARUSI YA PAUL OKOYE WA P SQUARE YAWEKWA WAZI

Maandalizi ya Harusi ya Paul Okoye
kutoka P Square pamoja na mpenzi
wake Anita Isama, ambayo itafanyika
tarehe 22 mwezi huu huko Port
Harcourt Nigeria, yameanza kushika
kasi ambapo mbali na mambo
mengine, zoezi la kusambaza kadi kwa
waalikwa maalum wa sherehe hii,
tayari limeshaanza.
Harusi hii inatarajiwa kuweka
rekodi nyingine ya aina yake, na hii
ni kutokana na dalili za awali
kabisa, ikianziwa na ufahari wa
kadi yenyewe ya harusi ambayo
tayari imekwishaonekana
hadharani.


0 comments:

Find us on facebook