contributor

MRADI MABASI YAENDAYO KWA KASI KUKAMILIKA 2015

Ujenzi wa daraja la Ubungo


Kituo cha basi kikiwa katika hatua ya mwisho kukamilisha ujenzi wake

Peter Mumuo (wa kwanza kushoto) akiwa na William Gatambi Meneja uhusiano wakala wa mabasi yaendayo kwa kasi Tanzania wakiwa kwenye kikao na Waandishi wa habari Posta Dares salaam

Wakala wa mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit – DART) ulioanzishwa na serikali tarehe 25 mei 2007. Wakala huu unaendelea na utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka ambao umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita.
Kwa mujibu wa Bwana William Gatambi meneja uhusiano wakala wa mabasi yaendayo kwa kasi amesema, awamu kwanza iko kwenye hatua ya ujenzi ambapo inatarajia kuisha mwezi june mwaka huu. Awamu ya pili na tatu bado inafanyiwa usanifu. Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi unarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma mwaka 2015 ambapo itahusisha mjumuisho wa awamu zote tokea ya kwanza mpaka ya mwisho. Baada ya wamu zote kukamilika mradi huu utaanza kutoa huduma kwa wananchi wa jiji la Dares salaam.
Miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi inajumuisha barabara ya kilometa 20.9 kuanzia Kimara mwisho hadi Kivukoni, ikijumuisha sehemu ya barabara ya Kawawa toka Morocco hadi Magomeni na barabara ya Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo,vituo vidogo 27,vituo vikuu 5 ,viuto mlisho 4 na karakana 2. Ujenzi wa miundombinu ya barabara unajumuisha njia za waenda kwa miguu na baiskeli.

0 comments:

Find us on facebook